Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amezindua Mradi wa Maji wa Kisiwa Kidogo Cha Jibondo Wilayani Mafia Mkoa wa Pwani.

Waziri Aweso aliambatana na Mhe. Omar Kipanga Mbunge wa Mafia na Naibu Waziri wa Elimu.


Mradi wa Maji wa Jibondo ni wa kipekee na mfano nchini kwakuwa umekatiza bahari kutoka Kisiwa cha Mafia kwenda Kisiwa kidogo Cha Jibondo umbali wa zaidi ya Km 7.8.

Mradi huu wa kihistoria umepokelewa kwa shangwe na furaha kubwa na wananchi wa Jibondo waliokumbwa na changamoto ya Maji kwa muda mrefu sana na kuaminishwa kwamba maji hayawezi kufika visiwani humo.

Mwisho wananchi wa Jibondo Wilaya ya Mafia wametoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikishia huduma muhimu ya Maji kupitia Wizara ya Maji.