Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Panolama Bw. Elizeus Gabriel kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mwendesha pikipiki (bodaboda) mkazi wa Kata ya Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera, alipokuwa akikatiza karibu na maduka ya wafanyabiashara majira ya usiku.

Eliudi Kijuzi ambaye ni kijana wa miaka 28 aliuawa kwa kupigwa risasi na wanaodaiwa kuwa walinzi wa kampuni ambao wanalinda maduka ya wafanyabiashara wa Nshamba Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.