Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amerejea nchini Tanzania baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Ubelgiji na Ufaransa.
Ziara yake ilianzia nchini Ufaransa katika mualiko wa mkutano wa bahari moja kwa dunia nzima, lengo lilikuwa ni kuona namna ya kutumia bahari katika sekta ya kiuchumi na kiulinzi.
Vilevile Rais Samia aliweza kufanya ziara ya kiserikali kwa kuwa na ziara na Rais Emmanuel Macron na kutembelea maeneo mbalimbali na kukutana na wafanyabiashara wa nchini humo.
Katika ziara hiyo rais amesema, walifanikiwa kupata pesa kidogo ambazo ni kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa barabara ya mwendo kasi na kuimarisha sekta ya kilimo.
Vile vile mabasi ya umeme ni suala ambalo waliligusia katika mazungumzo yao.
Aidha Rais Samia amesema anaona Tanzania itakuwa na mabadiliko makubwa katika miaka mitano au sita ijayo.
Lakini pia kuliwekwa mkataba wa marekebisho ya uwanja wa ndege za ndani ya nchi Terminal two, ambao ulijengwa na wafaransa hapo awali na sasa kumechakaa tayari.
Rais Samia amewadokeza wauza biashara ndogondogo kuwa kuna fedha kidogo zimevunwa kwa ajili yao.
"Imani yangu ni kwamba sekta binafsi ikiweza kuwekeza basi serikali haina haja, sekta binafsi ikiwekeza maendeleo yanakuja"
Rais Samia aliongeza juu ya kukwamua miradi mbalimbali ambayo ilikwamba njiani baada ya kutatizana na mataifa hayo ya ulaya, lakini sasa kazi itaendelea.
Vivyo hivyo kuna fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya Afrika.
Ziara hilo limezungumzia masuala ya amani, corona, usalama na uhamiaji.
Kwa upande wa Tanzania tayari wamevuna euro 425 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Na rais Samia alimaliza kwa kusema kuwa Watanzania wanaioshi ughaibuni watafanyia kazi masuala ya sera ya nje kwa kuwatambua ili waweze kuwekeza kwa kujiamini wakiwa nje ya nchi.
0 Comments