Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha wakulima wa Tumbaku Wetcu Ltd, Hamza Kitunga akizungumzia kuhusu masoko leo. Picha na Robert Kakwesi

  Chama Kikuu Cha wakulima wa Tumbaku,Wetcu ltd,kinatarajia kupitia wakulima wake kuuza zaidi ya kilo 16 milioni zenye thamani ya zaidi ya Sh55 bilioni.

Meneja mkuu wa Wetcu ltd,Samwel Jokea,amesema wanachama wake kupitia Vyama vya msingi 103 wamezalisha kilo 16.2milioni zinazotarajia kuwaingizia Sh58bilioni.

Kwa mujibu wa meneja mkuu Jokes,wastani wa kilo ya Tumbaku ni Dola ya Kimarekani 1.6 ambao utatumika katika Masoko ya tumbaku yanayoanza baadae mwezi huu.

Amesema kuwa Masoko ya Tumbaku yanatarajia kuanza tarehe mwezi huu na kuwa wakulima waanze kujiandaa kuuza Tumbaku Yao.

"Wanachama wetu wachangamkie Masoko yatakapoanza baadae mwezi huu kuuza Tumbaku Yao" Amesema.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha wakulima wa tumbaku,Wetcu ltd,Hamza Kitunga,amewataka wanachama wake kutochanganya madaraja Pamoja na kuzingatia ufungaji mzuri  ili wapate madaraja ya juu yenye bei nzuri.

Amesema lazima wajipange vizuri kupata madaraja mazuri ili mwisho wa siku wapate madaraja na malipo mazuri zaidi. "Tunawaomba kuelekea kipindi hiki Cha kuanza Masoko,wasichanganye madaraja ili malipo Yao yawe mazuri"Amesema

Chama kikuu cha wakulima wa tumbaku,Wetcu Ltd kina wanachama wa vyama vya msingi wapatao 130  ambao pia wanalima mazao mengine kama karanga, alizeti na pamba.