Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utendaji kazi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS), Aprili 8, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Bandari Tanzania, Eric Hamiss (katikati), wakati alipokagua utendaji kazi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS), Aprili 8, 2022. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Tanzania, Balozi. Ernest Mangu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa. Makame Mbarawa, Wandendaji wa Bandari ya Tanzania TICTS, na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Bandari jijini Dar es salaam, Aprili 8, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Meneja Usafirishaji na Ukaguzi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Injinia Said Mkwawa, wakati alipokagua utendaji kazi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS), Aprili 8, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) Matt Clift, wakati alipokagua utendaji kazi kwenye Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS), Aprili 8, 2022. Kulia ni Mkurugenzi wa Bandari Tanzania, Eric Hamiss. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) kuimarisha utendaji kazi wake ikiwemo kuacha kuchelewesha ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema kuwa kampuni hiyo ina paswa kufanya kazi kwa weledi na kupitia mkataba wa utendaji kazi wake ili kuhakikisha inatoa huduma stahili kwa wateja wanaohudumiwa na bandari hiyo na kuwa kimbilio.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Aprili 08, 2022) jijiji Dar es Salaam wakati alipozungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) na kukagua utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam kufuatia maagizo ya Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan..

“Tunataka mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu, bandari hii ndio injini ya uchumi wetu, hatutasita kufanya mapitio ya mkataba wa TICTS, wapo wawekezaji wengi ambao wana nia ya kuwekeza kwenye eneo hilo, hatuwezi kuvumilia kuona kuna ucheleweshwaji wa utoaji wa mizigo bandarini”

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Wizara itaendelea kuisimamia TPA ili kuhakikisha wanaendelea kupunguza zaidi na kwa wakati shehena yote inayopita kwenye bandari hiyo “Bandari ni sehemu muhimu kwenye uchumi wetu, tutahakikisha maeneo yote ambayo hayatumiki kuhifadhi mizigo yanaanza kutumika ili kuondoa msongamano”.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eric Hamisi amesema kuwa wameendelea kufanya maboresho katika bandari hiyo ili kuongeza ufanisi ikiwemo kununua vifaa vipya kama vile Reach Stracker Saba (7) na FolkLift mbili (2) za tani 16 kila moja.