JUMLA ya mabondia 32  leo Ijumaa wamepima audito  kwa ajili ya pambano la Usiku wa Kisasi linalotarajia tarajia kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar

 

Mabondia hao  wamepima uzito kwenye Uwanja wa Las Vegas uliopo Mabibo Sokoni jijini Dar tayari kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa na upinzani mkali kutoka kwa mabondia wa pande zote mbili.

Pambano hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Peak Time Media chini ya mkurugenzi wake, Meja Seleman Semunyu na kudhaminiwa na gazeti la  Spoti Xtra, +255 Global Radio, Bongo Boxing Safari, Creative Bee, Smartgin, Roby One Pharmacy, Clouds TV.

 

Katika pambano hilo, bondia Hamidu Kwata ambaye alikuwa anatarajia kucheza pambano kuu dhidi ya Ally Ngwando ameshindwa kutokea katika zoezi la kupima uzito kabla ya pambano hilo kesho Jumamosi.

 

Mratibu wa pambano hilo, Meja Seleman Semunyu alisema zoezi la uzito limeenda vizuri hivyo ni kesho wamashabiki wajitokeze katika pambano hilo.

“Kikubwa ni kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho katika pambano kwa kuwa masuala ya usalama yatakuwa vizuri lakini hata tiketi zimebakia chache katika gym za wadhamini, “alisema Khatibu.

 

Mbali ya wakali hao, wengine ambao watapima uzito ni msanii wa Twanga Pepeta, Kharid Chokoraa, Hamisi Molinyo na Emmanuel Mwakyembe, Khalid Chokoraa Chuma na Hassan Mandula na Tampela Maurusi na 

Wengine James Kibazange,  Ramadhan Kumbele,  Frank Yared  na  Mohamed Roboti, Hemed Rashid  na Ally Kilongola.