Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina wa msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo

JESHI la Polisi mkoa wa Arusha limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja anayesafirisha madawa ya kulevya aina mirungi katika jiji la Arusha.


Akitoa taarifa hiyo leo September Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina wa msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amekuwa tarehe 21.09.2022 muda wa saa 03:20 asubuhi huko maeneo ya Njiro katika Halmashauri ya Jiji la Arusha Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Benson Emmanuel (28) Mkazi wa Ngaramtoni, wilaya ya Arumeru  akiwa anakisafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi  magunia 10 yenye uzito kilogramu 155.8.