Mahakam ya Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara imemhukumu Charles Lemje (52), mkazi wa Kijiji cha Pori namba moja kwenda jela miaka 30 kwa kubaka mwanae wa miaka saba.

Mahakam ya Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara imemhukumu Charles Lemje (52), mkazi wa Kijiji cha Pori namba moja kwenda jela miaka 30 kwa kubaka mwanae wa miaka saba.

Kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, kwa tarehe tajwa tofauti hakimu amemtia mshtakiwa huyo hatiani kwa kosa la kubaka.

Kabla ya adhabu kutolewa hakimu alimtaka mshtakiwa kama ana chakuiomba mahakama hiyo ili impunguzie adhabu.

Mshtakiwa alimwomba hakimu ampunguzie adhabu kwa kuwa yeye ni mzee na hatoweza maisha ya gerezani.

Kwa upande wa mashtaka, walimwomba hakimu kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo kwa kuwa vitendo vya ubakaji Kiteto vimekithiri.

Hakimu Mosi Sasy kwa kuzingatia ombi la mshtakiwa, yeye ni mzee na kwa kuzingatia upande wa mashtaka kuwa ubakaji umekithiri Kiteto amemtia hatiani mtuhumiwa huyo kwenda jela miaka 30 akisema haki ya rufaa iko wazi ndani ya siku 30.