Wakuu wa nchi za Afrika wanakutana nchini Kenya kwa ajili ya mkutano wa kilele wa tabia nchi barani Afrika, ambapo watajadili mtazamo wa bara hilo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mkutano huo wa Nairobi ni wa kwanza wa aina yake barani Afrika unalenga kuja na mpango wa pamoja wa kuwasilisha kwa viongozi wengine wa dunia katika mkutano wa COP 28 wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa baadaye mwaka huu.
Katika siku tatu zijazo, wajumbe katika mkutano huo watazingatia mtindo mpya wa ufadhili ili kusaidia serikali kupunguza utoaji wa hewa ukaa.
Rais wa Kenya William Ruto alisema Afrika inapaswa kuwa sehemu ya suluhisho la ongezeko la joto duniani, badala ya kuwa mwathirika.
"Kwa muda mrefu sana tumeliona hili kama tatizo. Ni wakati wa kugeuza na kuangalia kutoka upande mwingine," aliwaambia wajumbe wakati wa ufunguzi wa mkutano.
"Kuna fursa, fursa kubwa pia. Na ndiyo maana hatuko hapa kuorodhesha malalamiko na kuorodhesha matatizo, tuko hapa kuchunguza mawazo, kutathmini mitazamo, ili tuweze kufungua ufumbuzi."
Nchi za Kiafrika ni miongoni mwa nchi zinazochangia zaidi mabadiliko ya hali ya hewa, lakini zinakabiliwa na baadhi ya athari zake mbaya zaidi

0 Comments