.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatazamiwa kuapishwa kwa muhula wa pili madarakani.

Matokeo rasmi yalimpa karibu 53% ya kura katika uchaguzi wa rais ambao waangalizi wa kimataifa walisema ulikosa viwango vya kidemokrasia.

Chama chake cha Zanu-PF kilipata karibu theluthi mbili ya kura za ubunge.

Mpinzani mkuu wa Bw Mnangagwa Nelson Chamisa ametaka uchaguzi mpya ufanyike.

Ana hadi Jumatatu kuiomba mahakama kubatilisha matokeo.

Wakati huo huo, kiongozi wa mapinduzi nchini Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema, anatarajiwa kuapishwa kama rais wa muda wa nchi hiyo.

Jeshi lilimpindua Rais Ali Bongo siku ya Jumatano muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliokuwa na utata.

Wafuasi wa uongozi wa kijeshi nchini Gabon wanatarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa Jenerali Nguema.

Hali nchini humo ni shwari lakini usalama umeimarishwa.

Kiongozi huyo wa mapinduzi anasemekana kuwa binamu wa Rais aliyeondolewa madarakani Ali Bongo, jambo linalozua shaka iwapo kweli hii inaashiria mwisho wa enzi ya miaka 55 ya Bongo.

Jenerali Nguema amesema hatakimbilia kuirejesha nchi kwa utawala wa kiraia, ili kuepuka makosa yaliyopita.

.
Image caption: Wanajeshi wa Gabon wakiwa tayari katika kuapishwa kwa kiongozi wa mapinduzi kama rais
.
.