EPL in Kenya

Rais William Ruto amepokea na kulikaribisha kombe la ligi kuu ya England (EPL) nchini Kenya, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Nairobi.

Kombe hilo lilisindikizwa na nguli wa soka Jay-Jay Okocha.

Baada ya kulipokea Rais Ruto alinukuliwa na vyombo vya habari vya ndani akisema: "Ligi kuu (EPL) inaleta msukumo kwa mamilioni ya wanasoka wanaochipukia kote duniani; Afrika, Kenya ikiwa ni miongoni mwao. Ni kivutio kikubwa cha soka".

Wachezaji kadhaa wa Kenya wamewahi kuchezea ligi hiyo pendwa akiwemo nahodha wa zamani wa Harambee Stars, Victor Wanyama, ambaye alizichezea Southampton na baadaye Tottenham Hotspurs na Divock Origi aliyekipigia Liverpool, mtoto wa nyota wa zamani wa Harambee Stars, Mike Origi.