Halaand

CHANZO CHA PICHA,

Manchester City wanatarajia kumpa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland mshahara mnono wa pauni 600,000 kwa wiki ikiwa ataongeza mkataba wake wa sasa unaomalizika mwaka 2027 wakitaka kumzuia kuhamia Real Madrid au ligi kuu ya Saudi. (Daily Star Sunday)

Katika siku ya mwisho ya usajili, Manchester City ilishindwa kutoa dau la £60m kwa ajili ya mshambuliaji wa Crystal Palace Eberechi Eze, huku The Eagles wakikataa kutoa pauni milioni 80 inayotakiwa kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka, 25. (Sunday Mirror)

Kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba anasakwa na vilabu vya ligi kuu ya Saudi vya Al-Ahli na Al-Ittihad, ambavo vyote vinaweza kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 30 wakati dirisha lao la uhamisho likiwa wazi. (Gazzetta dello Sport)

Pogba

CHANZO CHA PICHA

Maelezo ya picha,

Pogba

Al-Ittihad pia wamewasilisha pendekezo la mkataba kwa beki wa zamani wa Real Madrid na Paris St-Germain Sergio Ramos na wanasubiri jibu kutoka kwa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 37, ambaye pia anasakwa na klabu za Uturuki. (Fabrizio Romano)

Galatasaray wanaendelea na mazungumzo na Manchester United kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, baada ya ofa ya mkopo ya pauni milioni 1 kwa mchezaji huyo wa miaka 26 kukataliwa katika siku ya mwisho ya uhamisho. (Mail on Sunday)

Galatasaray wanatarajia kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, huku dirisha la uhamisho likiwa bado lliko wazi huko Uturuki. (Ajansspor, via Sabah)

Pierre-Emile Hojbjerg

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Pierre-Emile Hojbjerg

Tottenham inaweza kukubali kusitisha mkataba wa kipa Mfaransa Hugo Lloris ndani ya klabu hiyo mwaka mmoja kabla ya kumalizika baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 kushindwa kupata timu katika siku ya mwisho ya uhamisho baada ya ofa ya kwenda Newcastle United na Nice kuchelewa kufika. (Football Insider)

Rais wa Lazio Claudio Lotito anasema mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood alitaka kujiunga na klabu hiyo ya Italia lakini klabu hiyo ya Old Trafford haikukamilisha nyaraka kwa wakati kabla ya Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 21 kujiunga na Getafe kwa mkopo. (La Lazio Siamo Noi, via Mail on Sunday)

Mason Greenwood

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Mason Greenwood

Mshambulizi wa Uingereza Andre Gray, ambaye alivichezea vilabu vya Luton Town, Brentford, Burnley na Watford, anafuatiliwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kuondoka Aris Saloniki ya Ugiriki kwa makubaliano. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ubelgiji Yannick Carrasco, 29, atasafiri hadi Saudi Arabia kukamilisha uhamisho wa euro 15m kwenda Al-Shabab. (Fabrizio Romano)