Ligi kuu ya saudia huenda inaishinda ligi kuu ya Ufaransa , nahodha wa timu ya Brazil Neymar Jnr amesema.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alihamia katika ligi hiyo kutoka timu ya PSG mwezi Agosti kwa dau la £77.5m na marupuru.
Neymar alijiunga na Al Hilal katika dirisha la usajili ambapo klabu za saudia zilitumia Zaidi ya £700m kwa wachezaji wa kigeni.
‘’Kupitia majina ya wachezaji waliohamia Saudia, sitashangaa iwapo ligi ya Saudia ni bora kuliko ligi ya Ufaransa’’, alisema.
Matumizi ya Klabu za saudia katika uhamisho wa wachezaji dunianiulikuwa wa pili baada ya ligi kuu ya England ambapo klabu za ligi hiyo zilitumia takriban chini £1.6bkununua wachezaji wa kigeni , kulingana na takwimu za shirikisho la kandanda duniani Fifa.
Huku klabu ya Al – Ittihad ikishindwa kumshawishi mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salahkujiunga nao, baadhi wachezaji wa zamani wa klabu hiyo wakiwemo Jordan Henderson, Roberto Firmino na Fabinho ni miongoni mwa wachezaji kutoka ligi kuu ya England kuhamia Saudia.
Wachezaji maarufu waliohamia Saudia kutoka ligi ya Premia ni pamoja na:
Al-Ahli: Allan Saint-Maximin (Newcastle), Riyad Mahrez (Manchester City), Edouard Mendy (Chelsea), Roberto Firmino (Liverpool)
Al-Ettifaq: Jordan Henderson (Liverpool), Demarai Gray (Everton)
Al-Hilal: Ruben Neves (Wolves), Kalidou Koulibaly (Chelsea), Aleksandar Mitrovic (Fulham)
Al-Ittihad: N'Golo Kante (Chelsea), Fabinho (Liverpool)
Al-Nassr: Aymeric Laporte (Manchester City), Alex Telles (Manchester United)
Klabu za saudia pia zilimshawishi mchezaji mwenza wa Neymar katika klabu ya PSG Georginio Wijnaldum , na mshindi wat aji la Ballon d’Or karim Benzema na aliyekuwa mchezaji wa Bayern Munich Sadio Mane.

0 Comments