Wakenya na Watanzania kwenye mitandao ya kijamii wamejibizana kuhusu matamshi ya marais wao kuhusu raia wake wanaozungumza Kiswahili vizuri.
Kiswahili ndiyo lugha kuu inayozungumzwa katika mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki, lakini Wakenya mara nyingi wamekuwa wakidhihakiwa kwa kuhisiwa kutoweza kutumia Kiswahili sanifu huku Watanzania vivyo hivyo wakitaniwa kwa kutoweza kuzungumza Kiingereza fasaha.
Katika mkutano wa hivi karibuni wa kilimo na chakula nchini Tanzania, Rais Samia Hassan alim mwentania mwenzake wa Kenya William Ruto kwa kutotumia salamu inayofaa kwa Kiswahili.
“Juzi [Bw] Ruto alikuja hapa na kutufundisha kusema ‘jambo’, lakini jambo sahihi ni ‘habari ya mchana’. Wakenya hawa…tunahitaji kuwafundisha masomo ya Kiswahili,” alisema.
Lakini mwandishi wa CNN Larry Madowo, ambaye pia ni Mkenya na alikuwa mshereheshaji wa kongamano hilo, alimtetea rais wake.
“Lazima nimtetee rais wangu... kwa sababu Wakenya na Watanzania ni ndugu, tunazungumza na Watanzania kwa Kiswahili kibovu na Watanzania wanatujibu kwa Kiingereza kibovu, tunaendelea hivyo hivyo, kana kwamba ni injili,” alisema kwa Kiswahili, huku washiriki wakipiga makofi.
Mazungumzo hayo yaliangazia uhusiano wa kirafiki na utamaduni wa pamoja kati ya nchi jirani.

0 Comments