KAGERA; Karagwe. Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent L. Bashungwa ameungana na waumini wa Parokia teule ya Kayungu Jimbo Katoliki la Kayanga wilayani Karagwe kushiriki Misa Takatifu ya Pasaka, leo Machi 31, 2024.

Misa hiyo Takatifu imeongozwa na Padri Abdon Burondo, Mlezi wa Kituo cha Malezi Chabalisa ambapo wameshiriki waumini mbalimbali ikiwa ni pamoja na familia ya Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa ametumia nafasi hiyo kutoa salamu za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.