DAR ES SALAAM. RAIS Samia Suluhu Hassan amewatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Sikukuu ya Pasaka, huku akisisitiza umoja na mshikamano katika jamii.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Rais Samia ameandika: “Kheri ya Sikukuu ya Pasaka kwenu nyote. Katika siku hii ambayo ndugu zetu Wakristo wanaadhimisha kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo, tuendelee kujifunza katika upendo wake mkuu wa kujitoa kwa ajili ya wengine.
“Upendo kwa muumba wetu, utusukume kuishi katika njia iliyo njema. Upendo kwa ndugu, jamaa na jirani zetu, utusukume kuendelea kuliombea Taifa letu amani, umoja na mshikamano.
“Upendo kwa wale tunaotofautiana nao, utusukume kutafuta na kuishi katika maridhiano na ustahimilivu. Upendo kwa nchi yetu, utusukume kuitumikia kwa weledi na kila wakati kukusudia kupiga hatua mbele zaidi kwa kujenga upya.”
0 Comments