Rais wa Urusi Vladimir Putin anawania muhula wa tano madarakani.

Watu kote katika kanda 11 za saa za Urusi wamekuwa wakipiga kura kwa zaidi ya siku mbili na upigaji kura utakaa wazi hadi saa nane mchana kwa saa za hapa Jumapili.

Kura pia zinafanyika katika "maeneo mapya" ya Urusi - sehemu zinazokaliwa kwa mabavu za Ukraine ambazo sasa zinadhibitiwa na Urusi - huku vita dhidi ya jirani yake vikiendelea hadi mwaka wake wa tatu.

Urusi ilianzisha uvamizi wake kamili mnamo Februari 2022 na imekuwa kwenye vita na Ukraine tangu wakati huo.

Ingawa si jina la Putin pekee kwenye kura ya uchaguzi wa rais, hakuna shaka kwamba ataibuka mshindi.

Ikulu ya Kremlin imeondoa mazingira ya kisiasa, na kuwaondoa wapinzani wowote kwa mtu ambaye ameitawala Urusi, kama rais au waziri mkuu, kwa karibu robo karne.