Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Isaac Njenga amesema kila mmoja analo deni na jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba ana tunza mazingira kwa manufaa ya kizazi kijacho.

Amesema mazingira ambayo tunajivunia kwasasa ni sababu ya kuwapo kwa watangulizi ambao walijitoa kwa kupanda miti na kuitunza na leo inasaidia kuzalisha chakula, maji na mahitaji mengine.

Balozi Njenga ameyasema hayo leo Jumamosi Machi 16, 2024 wakati wa kupanda miti 300 katika Hifadhi ya Misitu ya Kazimzumbwi iliyoko wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Upandaji huo wa miti umeshirikisha Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Wangari Maathai inayoenda sambamba na siku ya Mazingira Afrika ambayo huadhimishwa Machi 3, kila mwaka.

Haata hivyo kwa mwaka huu siku hiyo ilisogezwa mbele baada ya msiba wa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia Februari 29, 2024.

“Tumeiadhimisha siku ya leo ya Wangari Maathai Day na siku ya Mazingira Afrika badala ya Machi 3, kutokana na msiba wa Mzee wetu, Hayati Ali Hassan Mwinyi, tunashukuru kuona kwamba kumekuwa na watu wengi kwani kutunza mazingira ni muhimu.

“Katika mambo ambayo Wangari alihimiza na kuzingatia ni kwamba sisi tuna wajibu kama kizazi kilichopo sasa kupanda mti ili kukisaidia ama kutunza mazingira na hali ya maisha ya vizazi vijavyo.

“Hivyo, kila mmoja wetu ana jukumu na deni la vizazi vijavyo katika utunzi wa mazingira, kwani haya tunayojivunia sasahivi ni sababu kulikuwa na watu waliopanda miti na kuitunza na ndiyo sasahivi tunapata maji, hali ya hewa nzuri na kupata chakula, hivyo hiyo ndiyo sababu inayotukutanisha katika siku yake na kuzingatia mambo aliyoyatilia mkazo siyo Kenya peke yake bali ukanda na dunia nzima kwa ujuma,” amesema Balozi Njenga.

Akimzungumzia zaidi Wangari, Balozi Njenga amemwelezea kama mtu esema: “Wangari maisha yake yote alizingatia utuanzaji wa mazingira maisha yake yote hadi kuwa mwananmke wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel kutokana na juhudi yake, mwaka 1977 alianzisha vuguvugu la kutetea mazingira (Greenberg Movement) kwa ajili ya kutetea haki za binadamu na kutunza mazingira,” amesema Balozi Njenga.

Awali, akizungumza katika siku hiyo iliyokuwa na kauli mbinu ya Panda mti, Okoa Dunia, Mwakilishi wa Kamishna wa Uhifadhi TFS, …amesema miti iliyopanda katika hifadhi hiyo ni inayostahimili ukame huku akiitaja baadhi kuwa ni migunga na mkangazi ambayo huoteshwa kando ya mto.

Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Immaculate Sware Semesi amesema mti ni mmoja ya kiungo cha dunia kinachoiwezesha kuishi kwani inaleta hewa, mvua, chakula na kulinda ardhi.

“Hivyo, siku ya leo tunaisherehekea hii siku kama Afrika ikiwamo Tanzania kwa mchango mkubwa wa Kenya ambayo inasimamia Jumuiya ya Kimataifa inayoshughulikia mazingira, pia tunamsherehekea Mama Wangari ambaye alikuwa kinara Tanzania kutokea Kenya katyika nyanja ya utunzaji wa mazingira na alikuwa kinara katika upandaji miti kwa mltu mmoja mmoja ndani ya Bara letu la Afrika na ni mwanamke wa kwanza kupewa tuzo ya Nobel rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa.

“Kama Afrika na familia ya Afrika lazima tuwe kinara kuhakikisha kwamba mazingira yetu yako safi, yako hai na tunashughulikia hali ya mabadiliko ya tabianchi, tunadhibiti hatari yakutokea kwa jangwa hivyo hali hii ikiendelea hivi ilivyo tutashindwa kuishi sababu mti ni uhai,” amesema Dk. Immaculata.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga akizungumza katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akiwa na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga, Naibu Kamishna Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bi.Carolen Mavunde pamoja na wadau wengine mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika mche mmoja wa mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga akizungumza katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga akizungumza katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akizungumza katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akiwa na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga, Naibu Kamishna Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bi.Carolen Mavunde pamoja na wadau wengine mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye picha ya pamoja katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Wadau mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)