Matthew Sussex, mtaalamu wa masuala ya Urusi pia profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha taifa cha Australia ameieleza BBC, kwa nini Islamic State inaweza kuishambulia Urusi – na lipi Urusi inaweza kufanya kujibu shambulio hilo.

"Urusi ina historia ndefu ya kutowatendea vema watu wengi waislamu waliopo nchini humo," ameiambia BBC.

"Tulikuwa na vita vya aina mbili huko Chechnya... vya pili mwakan 1999 hadi 2006 vilikuwa vita vya msimamo mkali ambapo ulikuwa na watu ambao walikwenda kupigana na Islamic State dhidi ya serikali ya Urusi.

"Tangu wakati huo, shughuli za Urusi nchini Syria zimewafanya Islamic State kuiona serikali ya Urusi kama tishio la kwanza."

Anasema anatarajia Urusi itajibu shambulio la ukumbi wa Crocus kwa “nguvu kubwa", akitolea mifano ya kilichofuata baada ya shambulio la tamasha la Moscow mwaka 2002 na shambulio la mwaka 2004 katika shule ya Beslan.

"Pengine, kwamba nani alifanya shambulio si jambo la muhimu lakini ni nani serikali ya Urusi itaamua kumlaumu na ni nani watamlenga katika kujibu shambulio"

Anasema onyo la Marekani la Machi 7, lililotelewa kuhusu uwezekano wa shambulio, lilichukuliw na na Ikulu ya Urusi maarufu Kremlin kama jaribio la “kuingilia” uchaguzi wa hivi karibuni na masuala yake ya ndani ya nchi.