Ibada ya wafu ya kijeshi inaandaliwa katika uwanja wa michezo wa Ulinzi, uliopo ndani ya kambi ya jeshi la nchi kavu nchini Kenya ya Langata. Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Ulinzi na rais wa taifa William Ruto anaongoza wanajeshi katika ibada hii maalum ya kijeshi kuwaomboleza wanajeshi kumi wlaiofariki kwenye ajali ya jeshi iliyotokea alhamisi aprili 18.

Katika baadhi ya sherehe ambazo zitakuwa tofauti na ibada za kiraia, itifaki na tamaduni za kijeshi zitaandaliwa kama heshima za mwisho kwa wanajeshi wenzao.

Miili ambayo ilikuwa inahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Mashujaa ya hospitali ya kijeshi ye Defence Forces memorial itasafirishwa hadi uwanjani ambapo majeneza na masanduku yatafunikwa kwa bendera ya Kenya.

Itakapowasili, gwaride ya heshima itaandaliwa kuwapa wanajeshi waliofariki heshima zao kuu, kisha miili itapeekwa raundi moja ndani ya uwanja ambapo wanajeshi watakaokuwa uwanjana watasaluti kama heshima za mwisho.

Baada ya ibada itakayoandaliwa na viongozi wa kijeshi ambao pia ni wa kidini, kutoka madhebebu ya katoliki, protestant na waislamu , kutakuwa na hotuba kutoka kwa viongozi wakuu wa kijeshi na kilele cha hotuba hizo ni ya Rais.

Baada ya hapo, tamaduni za kijeshi zitafanyika, tarumbeta itapigwa mara tatu ambayo inafahamika kama revile huku wote wakisimama na kunyamaza kimya kwa dakika moja. Baada ya hapo, tarumbeta nyingine italia huku ikipigwa kwa muda. Hatua hiyo inafahamika kama the last post na ina tumiw ana wanajeshi kuonyesh aishara kwamab wenzao wamefariki kazini, au vitani.

Kisha mizinga 19 itapigwa na jeshi la majini kama saluti ya mwisho kwa wanejshi waliowaacha , hali ambayo itachukuwa dakika kumi hivi.

Kabla ya miili kuondoka uwanjani, wanajeshi wa angani watajipanga katika msimamo unaofahamika ikama MISSING MAN FORMATION . ndege za kivita zitajipanga angaani kwa shepu ya V au pembe mbili .

Haya ni wakati maandalizi ya mazishi ya Jenerali Ogola yakiendelea, akiatarajiwa kuzikwa siku ya Jumapili huku maafisa wengine wawili waliofariki katika ajali hiyo wakizikwa siku ya Ijumaa

Rais William Ruto ameongoza ujumbe kutoka serikalini kuifariji familia ya Jenerali Ogola.