Katika kuendelea kutekeleza Azma ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia katika Taasisi za Serikali ikiwemo Magereza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini Mhandisi Hassan Saidy amesema wataiwezesha Magereza kwa asilimia 100 kununua Mashine 61 za kutengeneza mkaa mbadala.
Mhandisi Saidy ameeleza haya leo hii Jijini Dodoma katika Hafla ya utiaji saini Hati ya makubaliano ya Utekelezaji wa programu ya ujenzi wa miundombinu ya Nishati safi ya kupikia Magerezani kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
Na ameongeza kuwa inaleta maana sana kuona Taasisi za Serikali zinatangulia mbele katika ili wanachi kuweza kuelewa maana ya umuhimu wa Nishati safi ya kupikia.
"Tutaiwezesha Magereza kununua Mashine 61 za kutengeneza mkaa mbadala na hili Mwenyekiti na lenyewe halina kuchangia,nimeshaongea na anayehusika na Nishati safi amesema REA tutahusika kwa asilimia 100. Rea tutakuwa tukitoa hela ila taratibu zote zitakuwa zinafanya na Magereza ".
"Hili agizo limetoka serikalini na inaleta maana sana kuona Taasisi za Serikali zinatangulia mbele ili na sisi wananchi wa kawaida tuweze kuelewa maana ya Nishati safi ya kupikia ikienda mbele. Isingekuwa na maana kama huku tunawaambia wananchi wahame kutoka kwenye matumizi ya kuni na mkaa halafu Jeshi kubwa kama la Magereza ambalo tumeambiwa kiwango cha miti inayokatwa kwa matumizi ya kuni ni kikubwa bado wanabaki kukekule kwenye Nishati ya zama zamani,kwahiyo hili jambo ni jema pamoja na faida zake zilizosemwa ikiwemo kubotesha afya za wafungwa na watumishi wa Magereza "
Naye Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Mzee Ramadhani Nyamka ametumia wasaa huu kuwahakikishia REA kuwa atasimamia na kufuatilia matumizi ya fedha za ruzuku zinazotelewa na REA katika programu hii ili kutimiza Azma ya Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Napenda kuchukua fursa hii kutoa hakikisho kuwa nitasimamia na kufuatilia matumizi ya fedha za Ruzuku zilizotolewa na REA katika kutekeleza programu hii ili kutimiza Azma ya Mheshimiwa Raisi sambamba na kufikia malengo kwa ufanisi na tija iliyokusudiwa".
Awali akisoma taarifa fupi kuhusu Programu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia Magerezani ACP Kizito Jaka amesema lengo kuu la kugawa vifaa vya nishati mbadala katika Magereza kama vile majiko ya gesi ni kupunguza uchafuzi wa Mazingira pamoja na kuboresha afya za wafungwa na watumishi wa Magereza.
Mitambo itakayosimikwa katika Magereza zote 129 Nchini ni 126 ya Bayogesi,Mitambo 64 ya gesi ya kupikia ya Mitungi(LPG) na Mtambo 1 wa gesi ya asili (NG),Mashine 61 za kutengeneza mkaa mbadala na Mitungi 15,000 ya gesi ya kupikia ya Mitungi(LPG). c
0 Comments