Mshindi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon, Mkenya Kelvin Kiptum, ataenziwa katika mbio za London Marathon siku ya Jumapili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifariki pamoja na kocha wake, Gervais Hakizimana wa Rwanda, katika ajali ya gari magharibi mwa Kenya mwezi Februari.

Kiptum alipangiwa kushiriki katika mbio za London Marathon za mwaka huu, ambapo alikuwa akitazamia kushinda kwa mwaka wa pili mfululizo.

Tukio hilo litaanza kwa heshima kwa Kiptum.

"Tutakachokuwa tukifanya... ni kumsherehekea," mkurugenzi wa hafla Hugh Brasher alisema katika mahojiano na BBC Sport.

"Na tutakuwa tukitoa hotuba kabla na kuwataka washiriki wote kushiriki katika sekunde 30 za kumshangilia Kelvin - kwa maisha ambayo hatukuwa tunamjua, kwa mtu ambaye hatumjui, lakini pia kwa kile alichokipata, mafanikio, kwa mtu aliyekuwa na kwa kifo cha kusikitisha kilichotokea mapema mwaka huu."

Kiptum alikuwa ameweka rekodi katika mbio zote tatu za marathoni alizokimbia katika maisha yake ya muda mfupi.

Aliweka rekodi katika mbio za mwisho za London Marathon.

Muda mfupi baadaye, alikimbia mbio za marathon za kasi zaidi katika historia huko Chicago, akiweka rekodi ya kukimbia kwa 2:00.35.

Kiptum pia aliweka rekodi ya kukimb ia mbio za haraka zaidi za marathon katika mbio zake za kwanza za marathon huko Valencia.

Mbio za Rotterdam Marathon, ambapo Kiptum alipanga kukimbia, pia zilitoa heshima kwake Jumapili iliyopita.

Washiriki, akiwemo mke wa Kiptum Asenath Rotich, walishiriki katika tukio la kukaa kimya kwa dakika moja kwa heshima yake.