Waziri mkuu wa Israel anatarajiwa kukutana na maafisa wa ngazi za juu ili kujiandaa na uwezekano wa mashambulizi ya Iran, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Kuna hali ya wasiwasi kwamba Tehran italipiza kisasi shambulio la anga lililoua makamanda wakuu wa Iran karibu wiki mbili zilizopita.

Nchi kadhaa sasa zimewaonya raia wao kuhusu kusafiri katika nchi zote mbili.

Maafisa wa Marekani wameiambia CBS News, mshirika wa BBC wa Marekani, kwamba shambulio kubwa dhidi ya Israel linaweza kutokea mara moja.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anatarajiwa kukutana na wajumbe wa baraza lake la mawaziri wa vita, akiwemo Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant na kiongozi wa upinzani Benny Gantz.

Afisa mmoja wa Marekani CBS alizungumza na kuonya Iran inaweza kutumia zaidi ya drones 100, makumi ya makombora ya cruise na pengine makombora ya balestiki.

Haya yanaripotiwa kulenga shabaha za kijeshi nchini Israel katika shambulio ambalo ukubwa wake Israel itapata "changamoto" kujilinda dhidi yake.

Afisa huyo aliongeza kuwa bado kuna uwezekano Iran inaweza kuamua kujizuia.Chanzo cha pili pia kiliithibitishia CBS kwamba hatua ya Iran inaweza kutokea Ijumaa.

Waliweka idadi ya makombora ya cruise ambayo yanaweza kutumiwa na Iran kushambulia Israel kuwa 150 na kusema kiwango kilichopangwa cha shambulio hilo kimeongezeka katika siku za hivi karibuni - iliripotiwa kuhakikisha kuwa angalau baadhi ya droni na makombora yatapitia anga ya Israeli.