Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron amekuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu matukio ya mwishoni mwa wiki ambapo Iran ilifanya mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel.

Haya ndio mambo muhimu aliyoyasema:

  • Cameron hakuwa na shaka kwamba Israel ina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka kwa Iran - lakini alisema ushauri wa Uingereza sio kulipiza kisasi, akitoa wito kwa Israel kufikiria kwa "kichwa chake, na si kwa moyo wake"
  • Shambulio hilo kutoka kwa Iran lilikuwa "kushindwa mara mbili", kwa Iran -alisema, kwa sababu limeshindwa katika suala la uharibifu kwa Israeli na ilionyesha Iran kuwa "ushawishi mbaya katika eneo hilo"
  • Cameron alipongeza kuhusika kwa RAF katika kutungua ndege zisizo na rubani zilizokuwa zikielekea Israel Jumamosi usiku. Kama shambulio hilo lingefaulu, alisema, maelfu wangekufa
  • Alipoulizwa iwapo Uingereza imekuwa na ukali wa kutosha kwa Israel katika suala la kuwalinda raia wa Palestina huko Gaza, alisema juhudi za Uingereza zinalenga kuhakikisha mapiganoyanasitishwa na kupata misaada ya kuinia Gaza.