Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema madai ya Ukraine kwa nchi za Magharibi kuiruhusu kushambulia Urusi kwa silaha za Magharibi ni sawa na ulaghai, Reuters inaripoti.

Lavrov amenukuliwa na shirika la habari akisema akisema Urusi inapanua sheria zake kuhusu silaha za kinyuklia na kwamba ni hatari kwa mataifa ya Magharibi "kucheza na moto".

Rais wa Ukraine Zelensky amesema kuwa kutumia silaha zilizotengenezwa na nchi za Magharibi kushambulia maeneo ya ndani zaidi ya Urusi kutapunguza uwezo wa Moscow kushambulia Ukraine.