Rais William Ruto amemuidhinisha rasmi mpinzani wake wa muda mrefu Raila Odinga katika nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

Katika hafla iliyofanyika Ikulu, Nairobi Jumanne, Rais Ruto alionesha imani na uwezo wa Odinga kuongoza AUC kutokana na taaluma yake ya uongozi.

"Namuwasilisha kwako mwanasiasa mwenye maono ya mwanamajumuhi, kiogozi shupavu na mwenye busara, mtaalamu na mwanateknolojia pamoja na mwanasiasa mahiri na mhamasishaji mkongwe wa kuleta mabadiliko chanya.

Nina imani kuwa atafanya kila awezalo na kufanya kila linalowezekana ili kuleta mabadiliko chanya." kuifanya Afrika ijivunie na kuwa yenye nguvu," alisema.

Maelfu ya viongozi kutoka eneo la Afrika Mashariki wamemhakikishia Odinga uungwaji mkono wao.

Odinga pia ataungwa mkono na sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa Masuala ya Kigeni wa Kenya (PS) Korir Sing’oei na aliyekuwa Balozi wa Kenya nchini Marekani, Elkana Odembo.