Mahakama Kenya

Mahakama ya Juu nchini Kenya imetoa maagizo yanayozuia kwa muda sehemu za uamuzi wa Mahakama ya Rufaa uliosema kuwa Sheria ya Fedha, 2023, ni kinyume na katiba.

Uamuzi huu unajiri kufuatia rufaa iliyowasilishwa na waziri wa fedha, pamoja na maafisa wengine wanne wa serikali, dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Rufani.

Sheria ya Fedha ya mwaka 2023 iliyopitishwa mapema mwaka huu, ilipata pigo kubwa tarehe 31 mwezi Julai, 2024, wakati Mahakama ya Rufani iliposema inakiuka katiba kutokana na kasoro za kiuratibu katika utungaji wake.

Mchakato uliotumika kutunga Sheria hiyo ya Fedha ulitawala mijadala ya Mahakama ya Juu, hasa kiwango cha ushirikishwaji wa umma.

Mahakama ilikubali kwamba masuala haya yanahitaji uchunguzi wa ziada wa mahakama na yanapaswa kuchunguzwa kwa kina wakati wa kusikilizwa kikamilifu kwa rufaa.