Mshukiwa mkuu wa mauaji ya takriban wanawake 42 ambao miili yao ilitupwa katika kitongoji cha Kware, jijini Nairobi Kenya ametoroka kutoka kituo cha polisi jijini Nairobi.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyopatikana na Citizen Digital, mshukiwa Collins Jumaisi Khalusha alitoroka na Waeritrea wengine 12 waliokuwa wamezuiliwa katika kituo hicho kwa uhamiaji haramu.

Siku ya Jumanne, mwendo wa saa kumi na moja asubuhi, afisa mkuu, Konstebo Gerald Mutuku, alitembelea – mahabusu na meneja wa kantini ili kutoa kifungua kinywa kwa washukiwa.

Walipofungua mlango wa mahabusu, walishtuka baada ya kugundua kuwa washukiwa hao 13 wote walitoroka kwa kukata matundu ya waya kwenye uzio.

Khalusha alikuwa ndani ya chumba hicho akisubiri kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kesi hiyo.