MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fatma mwasa amesema mkoa huo utachukua hatua kali za kisheria kwa wahamiaji haramu ambao wamegangania kuishi mkoani Kagera kama watajaribu kuhujumu kwa namna yoyote uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema anatambua baadhi ya vibarua wamekuwa wakija kufanya kazi kwenye mashamba na kupata ajira za vibarua ndogondogo kutoka nchi jirani na baaadhi wamekuwa wakiwadanya wananchi kwa kuwapa fedha ndogondogo ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na vijiji.

Amesema kuwa serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa uchaguzi wa serikali za mitaa unawahusu Watanzania na sio wahamiaji au wageni kutoka nchi nyingine.

Amesema kuwa Kagera inakadiliwa kuwa na wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura wapatao 1,566,330 ikiwa wanawake ni 780,000 wanaume ni 816,527 huku vituko vya kupigia kura vikiwa 3,833

Amesema kuwa zoezi la uandikishaji litaanza Oktoba 11- 20, na zoezi la kuchukua fomu za uongozi litaanza Novemba 1-7 na kampeini za uchaguzi zitaanza tarehe 20-26 huku uchaguzi ukifanyanyoka Novemba 27 mwaka huu.