Kiongozi wa upinzani wa jamhuri inayojitangaza ya Somaliland, Abdirahman Mohamed Abdullahi, ameshinda uchaguzi wa rais wa eneo hilo.
Maarufu zaidi kama Irro, alishinda kwa asilimia 64 ya kura na kuwa rais wa sita wa Somaliland tangu ilipojitenga na Somalia mwaka 1991.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 69, spika wa zamani wa bunge la Somaliland, alimshinda rais wa sasa Musa Abdi Bihi, ambaye alipata 35% ya kura.
Bihi alikuwa ameongoza eneo hilo lililojitenga tangu 2017, lakini wakosoaji walielezea mtindo wake wa kutawala kama baba wa watoto wadogo na kuminya uhuru wa maoni ya umma wakati matatizo ya kiuchumi yalipodhoofisha thamani ya sarafu ya nchi hiyo.
Wanadiplomasia kutoka nchi tisa za Ulaya na Marekani walishuhudia kura hiyo tarehe 13 Novemba, ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika mwishoni mwa 2022.
0 Comments