MKURUGENZI Mkuu Mteule wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Kanda ya Afrika, Faustine Ndugulile atazikwa Desemba 3, Kigamboni Dar es Salaam.

Taarifa ya mabadiliko ya ratiba imetolewa na Ofisi ya Bunge la Tanzania.

Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni amefariki usiku wa kuamkia November 27,2024 nchini India. Awali ratiba ilionyesha kuwa Ndugulile angezikwa Desemba 2, 2024.