Kocha Mkuu wa Tanzania, Hemed Suleiman 'Morocco' ameiongoza timu hiyo ya taifa kutinga katika fainali za Mataifa ya Afrika AFCON baada ya kuichapa Guinea 1-0.

Tanzania imemaliza katika nafasi ya pili ya kundi H nyuma ya DRC ikiwa na alama 10.

Katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Morocco mwakani inatajwa kuwa huenda ikawa na msisimko mkubwa.

Nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki zilizofuzu ni Uganda na DRC.

AFCON 2025 itakuwa ya nne kwa Tanzania huku ikiwa tayari imejikatia tiketi ya kushiriki michuano hiyo kwa mwaka 2027 ambapo Tanzania atakuwa mwenyeji sambamba na Uganda pamoja na Kenya.