Donald Trump anasema anapanga kutangaza hali ya dharura ya kitaifa, ambayo itamruhusu kutumia wanajeshi
Rais mteule Donald Trump amethibitisha kwenye mtandao wake wa kijamii kuwa anapanga kutumia jeshi la Marekani kutekeleza operesheni ya kuwafukuza wahamiaji wasio na vibali nchini Marekani.
Siku ya Jumatatu, alichapisha kwenye mtandao wa "TRUTH!!!" akijibu maoni ya mhafidhina ambaye aliandika kwamba Trump atatangaza hali ya dharura ya kitaifa na kutumia jeshi kuongoza "mpango wa kuwahamisha watu wengi."
Katika kampeni, Trump aliahidi mara kwa mara kutumia Walinzi wa Kitaifa kuwasaidia maafisa wa Uhamiaji na Forodha (ICE), ili kutekeleza jukumu hilo.
Kauli ya hivi punde ya Trump inakuja huku kukiwa na maswali kuhusu jinsi atakavyotimiza ahadi yake ya kuwafurusha watu wengi katika historia ya Marekani.
Alisema ataanza kuwahamisha siku yake ya kwanza ofisini, ambayo itakuwa Januari 20, 2025.
Kauli ya Trump aliichapisha kwenye mtandao wake wa Truth mapema Jumatatu huku akiendelea kutangaza uteuzi katika nyadhifa muhimu katika utawala wake.
0 Comments