
Ibrahim Traoré alizaliwa Machi 14, 1988, ni afisa wa kijeshi wa Burkina Faso ambaye amekuwa kiongozi wa mpito wa nchi hiyo tangu mapinduzi ya Septemba 2022, yaliyomuondoa madarakani Rais wa mpito Paul-Henri Sandaogo Damiba.
Akiwa na umri wa miaka 36 tu, Traoré kwa sasa ni kiongozi wa pili mwenye umri mdogo zaidi duniani baada ya Waziri Mkuu wa Iceland, Kristrún Frostadóttir, na pia ndiye rais mwenye umri mdogo zaidi anayehudumu kwa sasa.
Traoré alijiunga na Jeshi la Burkina Faso mwaka 2009, na kuhitimu kutoka Chuo cha Kijeshi cha Georges-Namoano.
Traore dunia imemjua kutokana na staili yake ya kutetea wanyonge na kulinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya wananchi wote, bila woga wala kumuonea mtu.
0 Comments