Staa maarufu wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage

 

STAA maarufu wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage, amekiri kwamba anajutia uamuzi wake wa kuachana na mume wake, Tunji Balogun (Teebillz), na kuanzisha uhusiano na mwanaume mwingine.

Katika mahojiano yake na jarida la Elle South Africa, Tiwa alieleza kuwa kuachana na mume wake ndiyo moja ya makosa makubwa aliyowahi kufanya katika maisha yake.

“Nilimfanya mume wangu asijisikie kuwa mwanaume kwa sababu nilianza kutoka na mwanaume mwingine. Bado nampenda na najua nilimkosea, lakini nataka kurekebisha mambo na turudiane.”

Tunji Balogun (Teebillz)

Tiwa anafichua na kuongeza, ingawa alijua kuwa alifanya kosa kubwa, alijikuta akiguswa na hisia za kimapenzi kutoka kwa mwanaume mwingine ambaye alimhadaa kuacha ndoa yake ili awe na uhusiano naye.

Tiwa anasema hakutaka kumtenga Teebillz na hakuwahi kuhitaji talaka, lakini aliingia kwenye uhusiano mwingine kwa kuwa alikuwa na shinikizo la kimapenzi.


Hata hivyo, kwa sasa amekuwa na utambuzi kwamba sio rahisi kwa mwanamke aliyemwacha mumewe kuolewa na mwanaume mwingine. Anawaasa wanawake kuwa makini na maamuzi wanayoyafanya, na kuepuka kufanya makosa kama alivyofanya yeye.