MKURUGENZI wa Mji Mafinga, Fidelica Myovella amesema mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali ( Ufundi) Changarawe iliyopo Kata ya Upendo ipo katika hatua ya ukamilikaji na kwamba watahakikisha mafundi hawapati changamoto ya vifaa.

Mkurugenzi huyo amesema hayo alipofanya ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali( Ufundi)Changarawe.

ADVERTISEMENT

Amesema kuna baadhi ya majengo ambayo tayari yamekamilika katika miradi hii na kuna baadhi ya majengo yanaendelea kukamilishwa kwa hatua tuliyofikia yatakamilika kwa wakati.

“ Ndoto za Rais Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan ni kuona wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya Elimu nchini Tanzania, hivyo kuamua kuleta fedha nyingi katika Sekta hii, lazima tusimamie Miradi hii na kuhakikisha inakamilika kwa wakati,” amesema.