DAR ES SALAAM: WIKIENDI hii miamba ya soka nchini Yanga na Simba itakuwa na kibarua kizito katika michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ngazi ya klabu.
Yanga itakuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuikaribisha TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Simba ikiwa mjini Tunis, Tunisia kuivaa CS Sfaxien ya huko katika Kombe la Shirikisho (CAF).
Akizungumzia michezo hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amezitakia kila la heri timu hizo na kusema kuwa anaamini zitafanya vizuri na kusisitiza kuwa zawadi ya goli la mama pia litakuwepo.
0 Comments