SERIKALI imepongezwa kwa jitihada kubwa za kuendelea kuweka mazingira rafiki yanayomwezesha mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo na mitihani kwa ujumla.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Sisters, Stella Mnunduma amesema wanashuhudia serikali yao inavyoendelea kuweka mazingira rafiki kwenye sekta ya elimu.
Mnunduma amesema hayo katika ziara ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkaoni Mtwara Mwalimu Hassan Nyange alipotembelea shule mbili za sekondari katika manispaa hiyo ikiwemo Shule ya Sekondari ya Mtwara Sisters na Call and Vision.
Aidha mkurugenzi huyo wa manispaa ametembelea shule hizo kwa lengo la kuzungumza na wanafunzi kuhusu taaluma,maisha, uzalendo na kuwatia moyo wa kusoma kwa bidii ili kuukomboa mkoa na taifa kwa ujumla.
‘’Nakupongeza sana mkurugenzi kwa kitendo kikubwa ulichokifanya kuja kutembelea shuleni hapa na kunawatia moyo wanafunzi na walimu kwa ujumla hali itayopelekea kuongeza hamasa zaidi katika masomo na kuongeza ufaulu wa mkoa,”amesema Mnunduma.
Mwanafunzi kutoka Shuleni ya Sekondari ya Mtwara Sisters, Anastazia Gervais ameshukuru na kupongeza hatua hiyo ya mkurugenzi kutembelea shuleni kwao kuzungumza na wanafunzi kama sehemu ya kufatilia kwa ukaribu maendeleo yao ambapo kwao ni faraja kubwa.Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Call and Vision, Fakihi Jafar ameahidi kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao ili waendelee kuleta matokeo mazuri.
Naye Mkurugenzi wa manispaa hiyo, amesema amekuwa na utamaduni wa kuongea na wanafunzi mara kwa mara kwani lengo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wanafunzi hao kuhusu taaluma pamoja na suala zima la nidhamu mzuri shuleni.“Huu ni mwendelezo wa utamaduni wangu ambao ni wakawaida kabisa kupita kwenye shule za msingi na sekondari kuhakikisha kwamba wanafunzi wa mtwara manispaa wanakuwa wanafunzi wa tofauti kama vile kuwa wazalendo, nidhamu nzuri mashuleni na kuwa miongoni mwa watu wataokuja kuwa na tija kwenye taifa hili’’amesema Nyange
0 Comments