WANANCHI wa Kata ya Silaloda Tarafa ya Endagikot katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu mkoani Manyara wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia umeme ambapo leo umeweza kuwashwa rasmi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema utekelezaji wa mradi huo ni chachu ya maendeleo ya nchi na watu wake.


Miradi huo wa umeme Silaloda sekondari na zahanati umegharimu Sh milioni 146 zikiwa ni fedha zilizotolewa mwaka wa fedha 2023/2024.

Kaimu Meneja Wilaya ya Mbulu, Bura Nyoka amesema miradi huo utawanufaisha jamii vijiji jirani na taasisi za Shule ya Sekondari Silaloda na zahanati.