Rais wa Marekani Donald Trump akutana na Mfalme Abdullah wa Jordan katika Ikulu ya White House mjini Washington.
Mfalme wa Jordan Abdullah amepinga vikali pendekezo la Donald Trump la kuwahamisha Wapalestina katika nchi yake.
Hii ni baada yakukutana na Trump Jumanne , ambapo katika mtandao wake wa X alisema Jordan haikubaliani na kuwahamisha raia wa Palestina mjini Gaza na ukingo wa Magharibi.
Akielezea kauli yake kama msimamo wa mataifa yote ya kiarabu ambayo yalipendekezwa kuwapokea wagaza kipindi Marekani wanakarabati ukanda wa Gaza.
Mfalme huyo wa Jordan ambaye alikutana na Trump kwa mara ya kwanza tangu pendekezo la kudhibiti Gaza litangazwe rasmi huenda nchi yake ikafungiwa msaada na Trump hadi watakapokubali kuwachukua Wagaza haya ni kwa mujibu wa Rais Donald Trump.
Jordan ikiwa nchi iliyo na ukuruba na Marekani katika mataifa ya kiarabu inahifadhi Wapalestina wengi .
Ingawa Mfalme huyo aliwakubali kuwapa huduma za matibabu watoto 2,000 Wagaza, alisisitiza kukarabati upya Gaza na kusuluhisha mzozo wakiutu kunafaa kupatiwa kipau mbele na sio juhudi za kuwahamisha Wagaza.
Akiwa katika mkutano na Trump mfalme wa Jordan alikaa kimya wakati Rais wa Marekani alisisitiza kudhibiti Gaza akisema juhudi zake zita kazi huku Wagaza wakiishi maisha mazuri katika mataifa jirani.
0 Comments