Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaona kuwa ni "vigumu ngumu zaidi, kusema ukweli, kufanya kazi na Ukraine" kuliko Urusi katika majaribio ya kuleta amani kati ya mataifa hayo mawili.

Marekani "inafanya vizuri sana na Urusi", na "inaweza kuwa rahisi kufanya kazi na" Moscow kuliko Kyiv, Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval siku ya Ijumaa.

Saa kadhaa mapema, Trump alikuwa amesema "anazingatia sana" vikwazo vikubwa na ushuru kwa Urusi hadi usitishaji vita na Ukraine ufikiwe.

Wakati huohuo, Marekani imesitisha kwa muda upatikanaji wa picha za satelaiti kwa Ukraine , huduma inayotolewa na kampuni ya teknolojia ya anga ya juu Maxar aliiambia BBC Verify, baada ya Trump kuwa tayari kusitisha msaada wa kijeshi kwa nchi hiyo.

Hii inakuja wiki moja baada ya mazungumzo ya ajabu ya White House , ambapo Trump alimsuta Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa "kutoheshimu" Marekani.

Malumbano hayo ya hadharani yalifuatiwa wiki hii na Trump kusitisha misaada yote ya kijeshi ya Marekani na ushirikiano wa kijasusi na Kyiv .Urusi kisha ilifanya shambulio kubwa la kombora na ndege zisizo na rubani kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine Alhamisi usiku.