Corneille Nangaa (kushoto) ni mmoja wa viongozi wanaosakwa na serikali ya Rais Tchisekedi (kulia)
Wizara ya Sheria ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahidi kutoa dola milioni 5 kwa yeyote atakayesaidia kumkamata Corneille Nangaa, kiongozi wa muungano wa mto Kongo, Bertrand Bisimwa na Sultani Makenga - viongozi wa kiongozi wa kisiasa na kijeshi wa vuguvugu la Machi 23 (M23).
Watu wengine wawili ni waandishi wa habari wanaoishi uhamishoni, ambao pia wanalengwa , atakayewakamata akiahidiwa zawadi ya dola milioni 4.

Viongozi hao wa waasi walishtakiwa bila ya kuwepo mahakamani na kuhukumiwa adhabu ya kifo mwezi Agosti mwaka jana na mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa kwa uhalifu wa kivita, na kusababisha uasi na uhaini.
0 Comments