Washukiwa watatu wanasakwa baada ya watu 12 kujeruhiwa katika tukio la ufyaliaji risasi katika baa moja mjini Toronto, polisi nchini Canada wamesema.
Tukio hilo lilitokea saa nne na dakika 29 siku ya Ijumaa karibu na mtaa wa Scarborough, mashariki mwa Toronto.
Mamlaka ilisema watu sita walipata majeraha ya risasi na wengine kujeruhiwa na vifaa kama vile vioo vilivyovunjika. Hata hivyo majeraha hayakuwa ya kuhatarisha aisha.
Polisi wa Toronto walisema watu hao watatu waliingia kwenye baa hiyo na "kufyatua risasi kiholela". Walikuwa wamebeba bunduki na bastola.
Mkuu wa polisi Paul MacIntyre anasema nia ya kutekeleza tukio hilo “kwa sasa haijajulikana na tunaangalia uwezekano wa aina yoyote ule.”
Polisi walisema wanatumia rasilimali zote zilizopo kuwatafuta washukiwa hao.
0 Comments