Takriban watu 14 wameuawa na wengine kama 30 kujeruhiwa kufuatia wimbi la mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine usiku kucha.
Hiki ndicho unachopaswa kujua kuhusu mashambulizi hayo:
- Kumekuwa na wimbi jingine la mashambulizi ya anga ya Urusi dhidi ya Ukraine usiku kucha, huku takriban watu 14 wakiuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kote nchini.
- Watu 11 waliuawa katika shambulio katika mji wa Dobropillya katika mkoa wa Donetsk , na wengine watatu walikufa katika shambulio la ndege isiyo na rubani huko Kharkiv.
- Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema mashambulizi hayo ya anga yanaonyesha kuwa malengo ya Urusi katika vita hivyo "hayajabadilika".
- Zelensky aliongeza kuwa ni muhimu sana kuongeza vikwazo kwa Kremlin
- Shambulio hilo la usiku lilikuja saa chache baada ya Marekani kuthibitisha kuwa ilizuia Ukraine kupata picha za kibiashara za satelaiti , baada ya kusitisha msaada wa kijeshi na kijasusi mapema wiki hii.
- Ukraine imeendeleza mashambulizi yake dhidi ya Urusi, huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikisema kuwa ilizuia ndege zisizo na rubani 31 katika eneo lake jana usiku.
0 Comments