SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) kwa mara nyingine tena limeshinda tuzo ya the ”Most improved Organization” eneo la huduma kwa wateja iliyotolewa na Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management(CICM).
Tuzo hizo zimetolewa 28, Machi 2025 jijini Dar es Salaam ambapo shirika limepata tuzo hiyo baada ya kufanya maboresho ya kutumia njia za kidigitali kurahisisha mchakato wa maombi ya umeme na upatikanaji wa huduma kuwa mwepesi kwa wateja wake.

Tuzo za Tanzania Service excellence awards hutolewa kila mwaka na zinalenga kutambua Taasisi za Umma na binafsi zinazoimarisha na kuboresha huduma bora kwa wateja wake.
0 Comments