Mkuu wa biashara wa Umoja wa Ulaya alisema jumuiya hiyo yenye wanachama 27 imejitolea kufikia makubaliano ya kibiashara na Marekani kwa kuzingatia "heshima" na sio "vitisho".
Haya yanajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kutoza ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa zote zinazotumwa Marekani kutoka Umoja wa Ulaya.
"EU inajihusisha kikamilifu, imejitolea kufikia makubaliano ambayo yatawafaa wote wawili," Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya Maros Sefcovic alisema baada ya mazungumzo na Muwakilishi wa masuala ya Biashara wa Marekani Jamieson Greer na Waziri wa Biashara Howard Lutnick.
"Biashara ya EU na Marekani hailinganishwi na lazima iongozwe na kuheshimiana, si vitisho. Tuko tayari kutetea maslahi yetu."
0 Comments