WANANCHI katika Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara wameiopongeza serikali kwa kuendelea kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao ikiwemo ya barabara.
Hayo yamejiri leo (jana) Mei 23, 2025 wakati Mwenge wa Uhuru ulipowasili kwenye halmashauri hiyo na kupitia miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya zaidi Sh bilioni 1.4. ikiwemo mradi ujenzi wa barabara ya Nitekela – Nyundo ya kilomita 1.5 kwa kiwango cha lami.
Miradi mingine ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Nyundo, ujenzi wa Shule ya Msingi Nyundo ‘B’ ya mkondo mmoja, mradi wa maji Malamba, kugawa majiko ya gesi kwa wananchi na mingine ambapo utakimbizwa umbali wa takribani kilomita 150.2.
Kwa Upande wake mkazi wa kijiji cha Nitekela kwenye halmashauri hiyo, Bakari Lali amesema ujenzi wa mradi huo wa barabara ni faida kubwa kwao kwani utarahisisha kusafurisha mazao mbalimbali yanayozalishwa kwenye maeneo hayo ikiwemo zao la korosho na mengine.
Rashidi Ally, mkazi mwingine kwenye kijiji hicho cha Nitekela anasema kabla ya ujenzi huo barabara hiyo ilikuwa haipitiki kwani ilikuwa na mashimo mengi hasa kipindi cha mvua lakini sasa inapitika vizuri na wananchi hao wanafanya shughuli zao za maendeleo kwa urahaisi.
Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mjini, Abdallah Chikota amewapongeza wananchi wa kjijiji hicho cha Nitekela na vijiji jirani kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuupokea Mwenge huo uhuru na kukagua mradi wa ujenzi huo wa barabara kiwango cha lami.
“Haya mnayoyaona ni matunda ya Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kumaliza changamoto za vijijin ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, elimu na maji”amesema Chikota.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi amesema maendeleo makubwa yanayofanyika ni upendona heshima inayoweka na serikali pamoja na wananchi katika maeneo mbalimbali.
Aidha moja ya kipaumbele cha Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha anaboresha miundombinu ya sekta ya barabara ili kuweka mazingira mazuri kwa wananchi ikiwemo hiyo ya nitekela-nyundo.
Barabara hiyo inatekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijin na Mijini Nchini (TARURA) ambapo utekelezaji wake umefikia hatua mzuri.
0 Comments