SERIKALI kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) inatarajia kutumia zaidi ya Shs bilioni 3 kutekeleza ujenzi wa jengo jipya la Taaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, hatua hiyo inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi katika Chuo hicho kinachojipambanua katika kutoa wahitimu mahiri nyanja za mbalimbali.
Jengo hilo litakuwa na vifaa vya kisasa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na maabara ya kompyuta, hatua itakayochochea matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu.
Kwa kuzingatia usawa na ujumuishwaji, jengo hilo limewekewa miundombinu kuwezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kufikia maeneo mbalimbali kwa urahisi.
Ujenzi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu.
0 Comments