Mwanamuziki Beyoncé ametangazwa kuwa bilionea na Forbes, na kumfanya kuwa mwanamuziki wa tano kujiunga na orodha ya watu matajiri zaidi duniani.

Nyota huyo wa Marekani amejiunga na kundi la wanamuziki wenye utajiri wa tarakimu 10, akiwemo Taylor Swift, Rihanna, Bruce Springsteen na mumewe Jay-Z, ambao jarida hilo la biashara linawaorodhesha kuwa na utajiri wa dola bilioni 2.5 (£1.85bn) kila mmoja.

Mapema mwezi huu, Forbes ilikadiria utajiri wa Beyoncé kuwa dola milioni 800 (£593m) na kutabiri kwamba atakuwa bilionea kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ya mafanikio.

Ziara yake ya Renaissance World Tour ya mwaka 2023 iliingiza karibu dola milioni 600, na kumfanya kuwa mmoja wa watu mashuhuri wa muziki wa pop duniani pamoja na Taylor Swift.

Sehemu kubwa ya utajiri wake unatokana na shughuli zake za muziki.