Utawala wa Donald Trump umekuwa ukiimarisha usimamizi wa mipaka na sheria ya uhamiaji tangu siku yake ya kwanza katika Ikulu ya White House.

Wasafiri kutoka nchi 40 ambazo raia wake wanaweza kusafiri kwenda Marekani bila visa hivi karibuni wanaweza kuhitajika kutoa taarifa za akaunti za mitandao yao ya kijamii kwa miaka mitano iliyopita.

Pendekezo hili liko katika rasimu iliyochapishwa na Idara ya Ukaguzi wa Mpakani ya Marekani.

Sharti hili, kulingana na waandishi wa hati hiyo, litawahusu raia wa nchi hizo ambao wanaweza kuingia Marekani kwa kujaza fomu rahisi ya maombi ya ESTA (Mfumo wa Kielektroniki wa Idhini ya Usafiri) na kupokea jibu.

Takriban nchi 42 karibu nchi zote za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Uingereza, pamoja na Australia, Brunei, Chile, Israel, Japani, New Zealand, Qatar, Singapore, Korea Kusini na Taiwan.

Kibali cha ESTA ni halali kwa miaka miwili na kitatoa ruhusa kukaa Marekani kwa hadi siku 90 kwa ziara moja.

Utawala wa Donald Trump umekuwa ukiimarisha udhibiti wa mipaka na uhamiaji tangu siku yake ya kwanza kuingia Ikulu ya Marekani, akitaja lengo la kuimarisha usalama wa nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya kigeni ilianza kuchunguza akaunti za mitandao ya kijamii za wale wanaoomba visa ya Marekani mwishoni mwa Mei.

Wapinzani wa utawala huo wanasema hatua hiyo mpya itawakatisha tamaa baadhi ya watalii watarajiwa na pia kupunguza haki za kidijitali za wageni.